Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Pazi yaanza na kichapo Road to BAL 2024

PAZI BAL Pazi yaanza na kichapo Road to BAL 2024

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Wawakilishi wa nchi kwenye michuano ya kuwania kufuzu fainali za klabu bingwa Afrika kwa mchezo wa mpira wa kikapu (BAL), Pazi wameanza vibaya mchezo wao kwanza wakifungwa pointi 84-57.

Pazi imecheza mchezo huo wa kwanza kwenye kundi lao lenye timu nne ikiwemo Cape Town Tiger ya Afrika Kusini watakayocheza nayo kesho Jumatano pamoja na Dynamos ya Burundi watakayokutana nayo keshokutwa Alhamis.

Pazi inayofundishwa na kocha Henry Mwinuka ilionekana kuzidiwa katika robo zote nne za mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Ellis Park Arena, jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

Wapinzani wa Pazi katika robo nne hizo waliongoza kwa pointi 18-14, 43-35, 65-43 na kumaliza 84-57.

Mchezo mwingine uliochezwa leo ni Club Ferroviario da Beira iliyoshinda pointi 75-55 dhidi ya JBC.

Timu itakayofuzu hatua hii ya pili inayojulikana kama Ellite 16 itashiriki fainali hizo zitakazofanyika nchini Senegal (BAL 2024).

Chanzo: Mwanaspoti