Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Pazi mambo magumu, bado moja

PAZI BAL Pazi mambo magumu, bado moja

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Pazi jana usiku imepoteza mchezo wake dhidi ya Cape Town Tigers pointi 95-87 ikiwa ni mchezo wao wa pili wa kuwania kufuzu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mchezo wa mpira wa kikapu (BAL).

Mashindano hayo ambayo ni hatua ya pili ya kufuzu fainali hizo 'Ellite 16' zitakazofanyika nchini Senegal 2024 yanafanyika jijini Johannesburg, Afrika Kusini ambapo mechi ya kwanza Pazi ilifungwa na NBA Academy pointi 84-57.

Leo Alhamis, Novemba 23, 2023, Pazi itacheza mechi ya mwisho ya kundi lao B dhidi ya Dynamos ya Burundi mchezo utakaochezwa usiku kwenye uwanja wa Ellis Park Arena. Ikumbukwe hizi timu zilikutana katika mchezo wa awali wa kufuzu hatua ya pili uliofanyika jijini Dar es Salaam, Pazi ilishinda.

Mchezo wa leo wa Pazi na Dynamos utakuwa mgumu na wenye upinzani mkali kwani timu zote mbili zimepoteza michezo yote miwili na atakayeibuka mshindi wa mchezo huo ndiye atashika nafasi ya pili baada ya Cape Town Tigers inayoongoza kundi lao ikishinda mechi zake mbili.

NBA Academy Africa pia imeshinda michezo yake yote miwili dhidi ya Pazi kwa pointi 84-57 ikaifunga Dynamos pointi 76-71 leo inamalizana na Cape Town Tigers lakini hata akishinda haipo kwenye mbio za kuwania kufuzu BAL kwani yenyewe inatumia mashindano hayo kama maandalizi ya NBA Draft.

Kwa maana hiyo, kundi B ambalo Pazi ipo Cape Town inayoongoza itacheza na mshindi wa pili wa kundi A, na endapo Pazi akishinda mechi yao ya leo basi itacheza na mshindi wa kwanza wa kundi A.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Johannesburg, kocha msaidizi wa timu hiyo Mohamed Mbwana amesema kuwa; "Tulishindwa kutumia vizuri nafasi tulizopata, mechi ilikuwa ngumu hivyo kwasasa tunajipanga na mchezo wa baadaye ingawa nao hautakuwa rahisi kwani wapinzani wetu nao wamepoteza mechi zao mbili, hivyo ni mchezo mgumu kila mtu anataka hiyo nafasi ya kusonga mbele."

Chanzo: Mwanaspoti