Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Nyota wa kikapu Tanzania atua Marekani

Anjela Minja Anjela Minja

Wed, 20 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa timu ya taifa ya mpira wa kikapu chini ya miaka 17 na klabu ya Vijana Queens Anjela Minja anatarajiwa kuondoka leo alasiri Septemba 20, 2023 kwenda nchini Marekani baada ya kuchaguliwa na shule ya North Florida Education Institute kwa ajili ya masomo ya mpira wa kikapu.

Anjela mwenye miaka 17 na urefu wa futi 6.7 mwenye uwezo mkubwa aliyewahi kuwa mchezaji bora wa kuzuia wa Afrika chini ya miaka 17 nchini Misri, Haya ni mafanikio kwake na iwapo atafanya vizuri masomo yake atakuwa na nafasi ya kuja kucheza ligi ya wanawake ya WNBA.

Aidha Anjela akiwa na umri wa miaka 15 tuu ameweza kuwepo kwenye klabu ya Vijana Queens kwa misimu miwili mfululizo ambao ni mabingwa watetezi wa ligi ya mkoa ‘BD League’ na taifa ‘NBL’ chini ya kocha Kabrola Shomari ‘KB’.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live