Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Nyota wa Celtics wafikia rekodi ya NBA ya 1984

Y.jpeg Jaylen Brown kushoto na Jayson Tatum

Thu, 9 Jun 2022 Chanzo: eatv.tv

Jaylen Brown, Jayson Tatum na Marcus Smart ni wachezaji wa kwanza kufunga alama zaidi ya 20, Rebound 5 na assists 5 kwenye mchezo 1 wa fainali ya NBA. Tangu mwaka 1984 walipofanya hivyo Kareem Abdul-Jabbar, Magic Johnson and Michael Cooper.

Wachezaji hao wamefikia rekodi hiyo baada ya kukiongoza kikosi cha Boston Celtics kushinda mchezo wa 3 wa fainali ya Ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA Alfajiri ya leo kwa kuifunga Golden state worriors kwa alama 116 kwa 100 na kuongoza 2-1 katika michezo 3 iliyochezwa katika mfululizo wa michezo 7 ya Fainali.

Kwenye mchezo huu wachezaji hao watatu wa Boston Celtics wamefunga juu ya alama 20, ambapo Jason Tatum amefunga alama 26 ametoa pasi za kufunga (Assist) 9 na Rebound 6 Jaylen Brown amefunga alama 27 pasi za kufunga (Assist) 5 na Rebound 9 nae Murcus Smart amefunga alama 24 pasi za kufunga (Assist) 5 na Rebound 7.

Kwa upande wa Golden State worriors mchezaji nyota wa timu hiyo Stephen Curry amefunga alama 31 pasi za kufunga (Assist) 2 na Rebound 4, na Klay Thompson amefunga alama 25 pasi za kufunga (Assist) 3 na Rebound 3.

Chanzo: eatv.tv