Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Nike wasimama na Ja Morant

Ja Morant Ja Morant

Sat, 17 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya NIKE imetangaza kuwa watasimama na Ja Morant na wataendelea kum-support kufuatia adhabu ambayo amepewa na Kamisheni ya NBA kwa kosa la kuonesha bastola hadharani kwa mara ya pili ambapo nyota huyo wa Memphis Grizzlies amefungiwa mechi 25.

“Tutaendelea kumuunga mkono, ndani na nje ya uwanja.” lilisomeka kwa ufupi andiko la NIKE. Jana Ijumaa, Ja Morant alitoa maelezo yake kufuatia uamuzi huo ambapo aliomba radhi kwa NBA, timu yake ya Grizzlies, Kamishna wa NBA Adam Silver na wengine ambao walimpa nafasi ya kuwa nyota wa NBA.

Ja Morant ataikosa michezo 25 ya mwanzo kwenye msimu ujao wa Ligi ya NBA ambapo adhabu yake itakuwa bila malipo kwa kukiuka mwenendo wa Ligi hiyo.

Taarifa ya NBA ilisema “Morant alionekana akiwa na bastola kwenye gari kupitia LIVE video ya Instagram Mei 13, ikiwa ni miezi miwili tangu afungiwe michezo Nane bila malipo kwa kuonesha LIVE video March 4 ambapo alionesha bastola huku akiwa amelewa kwenye kumbi moja ya starehe.” - NBA

Chanzo: www.tanzaniaweb.live