Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

NBA yaingia Mkataba na Kenya, kufungua ofisi

NBA Contact NBA yaingia Mkataba na Kenya, kufungua ofisi

Mon, 25 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kenya imeingia makubaliano na Shirikisho la Mpira wa Kikapu nchini Marekani (NBA) kufungua ofisi nchini humo kwa lengo la kuendeleza mchezo huo.

Rais wa Kenya, William Ruto ameshuhudia utiaji saini huo ukiongozwa na Waziri wa Michezo nchini humo, Ababu Namwamba wakiwa New York nchini Marekani.

Msemaji wa Ikulu ya Kenya, Hussein Mohamed amesema makubaliano ya Kenya na NBA yanatarajiwa kukuza vipaji mashuleni na kwenye jamii chini ya mpango wa ‘Talanta Hela’ ikiwa ni pamoja na mafunzo ya makocha, maskauti pamoja na ujenzi wa viwanja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live