Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

NBA All-star ni vita ya ukanda, kinapigwa kesho

Steph Curry NBA 3 Stephen Curry

Sat, 17 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kesho Jumapili kwa saa za Marekani na alfajiri kuamkia keshokutwa Jumatatu kwa saa za Afrika Mashariki, ule mchezo mkali unaohusisha mastaa walioupiga mwingi zaidi kwenye ligi ndefu (regular season) katika Ligi ya Kikapu Marekani unachezwa katika Uwanja wa Gainbridge Fieldhouse mjini Indianapolis, Marekani.

Giannis Antetokounmpo

Uwanja huo upo katika Ukanda wa Mashariki ilipo timu ya kikapu ya Indiana Pacers ambapo timu ya Mashariki ina nafasi ya kuutumia vyema ukanda huo kuibuka na ushindi dhidi ya Ukanda wa Magharibi - mchezo unaowakutanisha manahodha LeBron James kwa Magharibi na Giannis Antetokounmpo kwa Mashariki.

Giannis atakuwa na masupastaa wa timu mbalimbali za NBA wakiwa ni pamoja na Damian Lillard, Joel Embiid (kaumia), Jason Tatum, Tyrese Haliburton, Bam Adebayo, Paolo Banchero, Jaylen Brown, Jalen Brunson, Tyrese Maxey, Donovan Mitchell na Julius Randle.

Upande Magharibi, supastaa Lebron atawaongoza mastaa wake kina Nikola Jokic, Kevin Durant, Luka Doncic, Shai Gilgeous-Alexander, Devin Booker, Stephen Curry, Anthony Davis, Anthony Edwards, Paul George, Kawhi Leonard na Karl-Anthony Towns.

Mchezo huo ni wa kwanza kupigwa katika mfumo wa uteuzi mpya ulioanza baada ya ule wa zamani ambao ulianza mwaka 2017.

Mchezo huo unatarajiwa kutoa rekodi kibao kwa ajili ya msimu huu wa Ligi ya Kikapu Marekani, ambapo mastaa watapambana kuvunja zilizowekwa miaka ya zamani na wakongwe waliostaafu au wachezaji wanaoendelea kucheza kwa sasa. Hivyo sio mchezo wa kukosa - tukio ambalo litaanza kwa ratiba mbalimbali kuanzia saa 5:30 usiku kesho.

CURRY VS SABRINA

Mchuano mkali unaosubiriwa kwa hamu wikiendi hii ya mchezo wa All-star unajumuisha pia utamu baina ya wakali wawili wa kutupia pointi tatu kwenye ligi zote mbili za kikapu upande wa wanaume (NBA) na ile ya wanawake (WNBA).

Ni wakali Steph Curry anayetajwa kuwa mkali zaidi kwa muda wote kwenye historia ya NBA hususan katika upande wa kutupia pointi tatu dhidi ya Sabrina Lonescu anayetisha kwenye ligi ya upande wa wanawake nchini humo.

Wote wawili wameshawahi kushindana binafsi kwenye kurusha pointi tatu, lakini safari hii wanakwenda kusisimua zaidi kwa kushindanishwa hadharani na dunia itashuhudia nani ambaye anakwenda kumfunika mwenzake kuwania ushindi na ukali wa kutupia pointi hizo.

Chanzo: Mwanaspoti