Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Mjapani ateseka kwa Wembanyama

Victor Wembanyama F Victor Wembanyama

Thu, 1 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Victor Wembanyama amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya picha inayomwonyesha akikabwa na mchezaji mfupi kwa zaidi ya futi mbili katika mchezo wa mpira wa kikapu kwenye mashindano ya Olimpiki.

Staa huyo bora kabisa wa mwaka kwenye ligi ya NBA, Wembanyama, 20, aliichezea Ufaransa katika mechi ya pili ya mashindano hayo ya Olimpiki dhidi ya Japan juzi Jumanne.

Ilionekana kuwa mechi ngumu kwa Wembanyama, Rudy Gobert na wachezaji wenzao, kutokana na wakali wa Japan, Rui Hachimura na Yuki Kawamura kucheza kwa kiwango bora sana uwanjani.

Kawamura alifunga pointi 29 kwenye mchezo huo sambamba na ribaundi saba, huku akiasisti mara sita. Kwa kufanya hivyo, amekuwa mchezaji wa tatu kwenye karne hii kupiga zaidi ya asisti 25, ribaundi tano na asisti tano kwenye Olimpiki kwa mujibu wa FIBA.

Mchezaji mwenzake, Hachimura alifunga pointi 24 kwa timu hiyo ya Japan, ambapo licha ya jitihada zao, bado ilipoteza mechi kwa pointi 94-90.

Hata hivyo, mchezaji mwenye kimo cha futi 5 na inchi 6, Yuki Togashi, aliyecheza dakika 12 akitokea benchini kwa upande wa Japan, ndiye aliyekuwa gumzo.

Kilichomfanya awe gumzo ni kitendo cha kwenda kumkaba mchezaji mwenye futi 7 na inchi 4, Wembanyama na kuwaacha hoi mashabiki kutokana na tofauti yao ya urefu wachezaji hao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live