Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Mjane wa Kobe Bryant alipwa sh bilioni 37

 Vanessa Bryant.jpeg Mjane wa Kobe Bryant alipwa sh bilioni 37

Thu, 25 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya picha za mwili wa aliyekua nyota wa mpira wa kikapu wa Marekani Kobe Bryant kuvujishwa na naibu afisa wa polisi ambaye alisambaza picha hizo kwenye mitandao, mahakama imeamuru Mke wa marehemu Kobe alipwe dola milioni 16 (sawa na Tsh bilioni 37.3) kama fidia kutokana na kuvuja kwa picha hizo.

Mke wa wa Kobe, Bi Vanessa Bryant alitoa ushahidi huku akibubujikwa na machozi wakati wa kesi hiyo katika siku 11 alisema kwamba habari za picha hizo zilizidisha huzuni yake baada ya kumpoteza mumewe na bintiye kwenye ajali hiyo iliyotokea 2020.

Alipokua akishuhudia kuhusu tukio hilo amesema tukio hilo limemfedhehesha sana na kumfanya aingiwe na uoga,picha hizo zilionyesha mwili wa marehemu kobe.

“Nilihisi kutaka kukimbia na kwenda kujitupa kwenye maji na kupiga kelele, tatizo siwezi kukataa uhalisia wangu siwezi kuukimbia mwili wangu,” alisema Bi Bryant.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live