Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Michael Jordan aweka rekodi ya kukusanya viatu vyake

Utajiri Wa Michael Jordan Ni Trilioni 2.5 Michael Jordan aweka rekodi ya kukusanya viatu vyake

Sun, 4 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Aliyekuwa mchezaji wa mpira wa kikapu NBA kutoka nchini Marekani #Michael Jordani ameweka rekodi ya kukusanya viatu vyake alivyo wahi kuvivaa katika fainali ya sita za ‘The Dynasty Collection’ mwaka 1991 na kuviuza katika mnada wa #Sotheby kwa dola 8 milioni sawa na tsh 20 bilioni.

Kwa mujibu wa Business Insider inaelezwa kuwa viatu hivyo vya bei ghali zaidi vilivyowahi kupigwa mnada ambapo vilikuwepo viatu alivyo wahi kuvivaa katika ubingwa wa kwanza katika mchezo huo mwaka 1991 hadi fainali yake mwaka1998, vyote vikiwa na mpangilio wa rangi nyeusi na nyekundu.

Licha ya kustaafu mwaka 2003 Michael Jordan ambaye ana umuri wa miaka 60 anachukuliwa kuwa mchezaji bora katika NBA hadi sasa, Pia ndiye mchezaji basketball tajiri ambaye amejitengenezea kazi nzuri kwa kutumia utajiri wake kutoa misaada mbalimbali.

Chanzo: Bbc