Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Makocha 10 wamkubali Mtunguja

Agfrtsdhyt Makocha 10 wamkubali Mtunguja

Fri, 21 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya Stanley Mtunguja kuonyesha kiwango cha juu katika mashindano ya kanda ya tano ya Afrika umri wa miaka 18 nchini Uganda, makocha zaidi ya 10 wamevutiwa naye.

Kamishina wa makocha wa Shirikisho la mpira wa kikapu nchini (TBF), Robert Manyerere, alisema taarifa walizozipata kutoka Uganda makocha hao walianza kumshawishi mchezaji huyo ajiunge na timu zao.

“Tulichofanya tuliwasiliana na meneja wa timu ya taifa aliyekuwa Uganda na timu hiyo Aloyce Renatus, tulimweleza awaeleze makocha hao wafuate taratibu,” alisema Manyerere.

Mtunguja alianza kujifunza mchezo wa kikapu katika kituo cha Ukonga Academy, chini ya makocha Denisi Lipiki na Benjamini Ngogo.

Baada ya hapo alipandishwa kuchezea timu ya Ukonga Warriors kwenye ligi ya BDL na mafanikio yalivyozidi kuonekana akapandishwa kuchezea timu ya kwanza ya Ukonga Kings.

Kwa upande wa Lipiki, anasema anajua kijana wake anafuatiliwa na makocha mbalimbali, kwa upande wao amedai hawana tatizo kwa timu yeyote inayomuhitaji.

Lipiki ambaye ndiye kocha aliyemfundisha tangu akiwa mdogo, alishauri makocha wanaomuitaji wafuate taratibu.

Katika ligi ya BDL Mtungunja anaongoza kwa kutoa asisti akifanya hivyo mara 89, kwa upande wa ufungaji anashika nafasi ya pili kwa akipachika pointi 262, huku nafasi ya kwanza ikishikwa na Amin Mkosa wa timu ya Mchenga Stars aliyefunga pointi 294.

Chanzo: Mwanaspoti