Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Lebron amtoa KD kiaina

Yunr0pxh6xqlj4snyq04 Lebron amtoa KD kiaina

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Leo Jumatano timu ya mpira wa kikapu ya Marekani inatarajiwa kucheza mchezo wa pili mgumu dhidi ya Sudan Kusini katika mwendelezo wa mechi za Olimpiki nchini Ufaransa.

Ndani ya kikosi cha Marekani mashabiki wa kikapu duniani wanaweza kuwa watawatazama kwa mara ya mwisho wachezaji LeBron James, Steph Curry na Kevin Durant ‘KD’ wakichezea taifa hilo na kuwaachia nyota wengine, na hapo ndipo ilipo raha ya kushuhudia kinachofanywa na mastaa hao.

LeBron na Durant waliirahisishia kazi Marekani mbele ya Serbia ya Nikola Jokic ambaye uwepo wake unaifanya kuwa timu tishio, lakini siyo mbele ya Marekani iliyokuwa na KD na LeBron.

Kipindi cha kwanza pekee kilimtosha KD kufunga zaidi ya pointi 20 huku LeBron akikamilisha kazi wakiungana kufunga pointi 43, stori ikawa ni mshangao wa LeBron.

LeBron ambaye ndiye mchezaji kiongozi wa Marekani alishangazwa na kipaji chenye ubora cha KD kiasi cha kusema staa huyo siyo wa dunia hii, bali ana kipaji kisicho na mfanano hapa duniani.

Sainz amuachia kiti Hamilton

LILIKUWA ni suala la muda tu kabla ya dereva Carlos Sainz kuondoka kwenye kampuni ya Ferrari baada ya msimu huu kwisha, kwani hatimaye imethibitika amejiunga na Williams kwa miaka miwili kuanzia mwakani.

Sainz anapishwa na Logan Sargeant ambaye anakaa pembeni ili kumuachia vyema nafasi kujinafasi kuipeleka juu kampuni hiyo.

Kabla ya kusaini Williams, kampuni ya Sauber na Alpine zilikuwa zinamuwinda Sainz, lakini ni Williams waliofanikiwa kumnasa na kwenda kutengeneza combo pamoja na Alex Albon.

Msimu ujao Ferrari watakuwa na Lewis Hamilton ambaye ataachana na Mercedes huku akiwa amechachamaa kwa kushinda mechi mbili mfululizo.

Nadal, Djokovic mwisho wa enzi

UKITUMIA neno mwisho wa enzi kwa mastaa wa tenisi duniani, Rafael Nadal na Novak Djokovic hutakosea baada ya mchezo waliocheza Jumatatu jioni.

Ulikuwa ni mchezo wa raundi ya pili ya michuano ya Olimpiki ambapo wapinzani hao wakubwa waliumana kusaka mshindi wa kusonga hatua ya tatu na kikapigika vyema.

Alikuwa ni Djokovic kwa mara nyingine aliyeongeza rekodi ya kumchapa Nadal kuwa 31-29 akimzidi mbili na kumnyima fursa ya kumfikia - idadi ikiwa ni mechi 60 walizocheza.

Licha ya Nadal kushinda fainali tano katika tisa walizokutana, inawezekana ukawa mwisho wa enzi baina yao kukutana hasa katika michuano mikubwa ya taji la Grand Slam duniani.

Chanzo: Mwanaspoti