Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Lebron James afikiria kuachana na Kikapu

Lakers Nuggets Basketball 80293 Scaled E1684819115201 Staa wa LA Lakers, Lebron James

Tue, 23 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuchapwa fagio na Denver Nuggets alfajiri ya leo na kushuhudia timu yake Los Angeles Lakers ikishindwa kuingia fainali ya NBA mwaka huu, LeBron James anafikiria kustaafu mchezo wa Kikapu.

Akiongea na waandishi baada ya mchezo, LeBron alimaliza mkutano huo kwa kusema “Kuendelea na mchezo wa Kikapu, nina mengi ya Kufikiria.”

Alienda mbali zaidi na kufafanua kauli hiyo akisema;

“Nitafikiria kama nitaendelea kucheza, hasa mwakani.” alisema James (38) ambaye amekamilisha misimu 20 ya NBA.

Una lipi la kusema kuhusu uamuzi huu wa LeBron James?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live