Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

LeBron bado 400 avunje rekodi NBA

Le Bron James Jpg LeBron James

Fri, 13 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Akiwa na miaka 38 sasa, supastaa wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), LeBron James amebakiwa na pointi 400 ili kufikia rekodi ya muda wote ya pointi za msimu mrefu wa ligi (regular season) ya gwiji, Kareem Abdul-Jabbar aliyoiacha tangu mwaka 1984.

Kareem aliacha rekodi hiyo ya pointi 38,387 ambapo mchezaji aliye karibu zaidi kuifikia kwa sasa ni LeBron wa Los Angeles Lakers ambaye kabla ya mchezo dhidi ya Denver Nuggets jana Jumatano, alikuwa na pointi 37,965 huku kila mchezo akiwa na wastani wa kufunga pointi 27 na zaidi.

Kama LeBron ataendelea kufunga idadi hiyo ya pointi kwenye mechi 15 zijazo, anaweza kuvunja rekodi hiyo kabla ya mchezo wa Februari 09 dhidi ya Milwaukee Bucks endapo hataumia na kukosa mechi zijazo kwa timu yake.

Hii inamaanisha kwamba, LeBron anakwenda kuweka rekodi mpya na ya aina yake baada ya kuzivunja rekodi nyingi alizozikuta na sasa hii ya idadi kubwa zaidi ya pointi kwenye ligi ndefu anaenda kuivunja baada ya kutoka chini hadi kubakiwa na chini ya pointi 400 kuifikia.

Chanzo: Mwanaspoti