Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

LeBron James afikira kustaafu kikapu

Lebron James Vs Memphis LeBron James afikira kustaafu kikapu

Tue, 2 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa mpira wa kikapu kutoka nchini #Marekani anayekipiga #NBA, LeBron James (39) ameweka wazi kuwa anampango wa kupumzika kucheza mchezo huo.

#LeBron ameyasema hayo wakati akiwa kwenye mahojiano ya hivi karibuni ambapo alieleza kuwa muda si mrefu hatocheza tena kwani miaka 21 dimbani inamtosha, japo hajui ni lini atatangaza kustaafu kwake rasmi, lakini amedai kuwa atafanya hivyo muda si mrefu.

#LeBron alianza rasmi kucheza mpira kikapu mwaka 2003 ambapo alikuwa akikipiga katika ‘timu’ ya ‘Cleveland Cavaliers’ na sasa anachezea ‘timu’ ya ‘Los Angeles Lakers’ aliyosaini nayo mkataba toka mwaka 2018.

Hata hivyo ndani ya miaka 21 mchezaji huyo amewahi kuondoka na Tuzo kadhaa kutokana na makubwa aliyoyafanya katika mchezo huyo zikiwemo ‘NBA All-Star Game Kobe Bryant MVP Award’, ‘Best Record-Breaking Performance ESPY’, ‘USA Basketball Male Athlete of the Year’, ‘Mr. Basketball USA’ na nyinginezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live