Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Lakers yalipa kisasi kwa Clippers

LA Lakers X Clippers Lakers yalipa kisasi kwa Clippers

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Timu za Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani (NBA), Los Angeles Lakers na Los Angeles Clippers zinazotoka jiji moja la Los Angeles zimeendeleza dabi lao na safari hii Lakers imelipa kisasi kwa wapinzania wao hao.

Baada ya msimu uliopita wa ligi ndefu ya NBA (regular season), Clippers kuonyesha ubabe wake kwa Lakers ikishinda echi zote nne, msimu huu imeangukia pua kwa Lakers inayoongozwa na LeBron James kwa kuchapwa mechi mbili hadi sasa.

Lakers ilianza kwa ushindi wa pointi 130-125, Novemba mwaka jana na juzi Jumatatu ikashinda pointi 106-103, LeBron akiongoza maangamizi.

Mechi mbili zilizobaki ambazo Lakers ana kazi ya kulipa kisasi cha msimu uliopita, zitachezwa Januari 24 na Februari 29 kukamilisha mechi nne za ndani ya msimu na kusubiri hatma ya kama zitakutana kwenye hatua ya mtoano (playoffs) zote zikiwa Ukanda wa Magharibi.

Chanzo: Mwanaspoti