Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

LA Lakers wapoteza Fainali ya Pili

Lakers Lost To Denver LA Lakers wapoteza Finali ya Pili

Fri, 19 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Los Angeles Lakers alfajiri ya leo imepoteza mchezo wa fainali ya pili ya ligi kuu ya kulipwa ya mpira wa kikapu Marekani (NBA) Kanda ya Magharibi, kwa kipigo cha pointi 108-103 kutoka kwa Denver Nuggets.

Mchezo wa fainali ya kwanza ya Magharibi uliopigwa siku ya Jumatano Denver ilishinda kwa pointi 132-126.

Si matokeo mazuri Kwa Lakers ya mkali Lebron James lakini pia si matokeo mabaya kwao, Kwa vile walikuwa ugenini ambapo Jumapili hii na Jumanne watacheza fainali ya tatu na ya nne uwanja wao wa nyumbani.

Fainali ya upande wa Mashariki, Miami Heat wanaongoza baada ya ushindi walioupata katika fainali ya Kwanza Kwa pointi 123-116, huku alfajiri ya kesho wakicheza fainali ya pili.

Ikumbukwe mshindi wa jumla wa fainali ya Kanda ya Magharibi na mshindi wa jumla wa fainali ya kanda ya Mashariki, watachuana ili kumpata Bingwa wa jumla wa NBA 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live