Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Hasheem aita mashabiki

PAZI BAL Hasheem aita mashabiki

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Nyota wa kimataifa wa mpira wa kikapu nchini anayeichezea Pazi, Hasheem Thabeet amewaomba Watanzania wanaoishi Afrika Kusini kujitokeza kwa wingi na kuwapa sapoti watakapokuwa nchini humo.

Pazi inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mchezo huo (BAL) hatua ya pili baada ya kufuzu hatua ya kwanza iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Pazi inatarajia kuondoka usiku wa kuamkia kesho Jumapili kwenda Sauzi kuwahi mashindano hayo yanayoanza Novemba 20 ambapo Pazi itacheza mechi yake ya kwanza siku inayofuata dhidi ya Dynamos.

Akizungumza na Mwanaspoti, Thabeet alisema mashindano hayo ni magumu ila anaamini watapambana ili kucheza fainali hizo hapo baadaye nchini Senegal.

“Tunahitaji sana sapoti ya Watanzania wote waliopo hapa na huko Afrika Kusini, maana kule tutakuwa pekee yetu hivyo waliopo Afrika Kusini waje kwa wingi kutusapoti,” amesema Thabeet.

Kauli hiyo imeungwa mkono na Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Damas Ndumbaro aliyesema: “Naaigiza Baraza la Michezo Tanzania (BMT), kuwasiliana haraka na ubalozi wa Tanzania huko Afrika Kusini kuipokea timu na kuwa nayo sambamba kwa muda wote watakaokuwa hapo.

“Ubalozi uhakikishe unawahamasisha Watanzania waliopo huko kujitokeza kwa wingi kusapoti timu,” alisema Dk Ndumbaro.

Chanzo: Mwanaspoti