Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Hasheem Thabeet arejea kukichafua Bongo

HASHEEM 1 Hasheem Thabeet

Sat, 23 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji nyota wa mpira wa kikapu Mtanzania Hasheem Thabeet amerejea nchini kujumuika na timu ya @pazibasketball ambayo inajiandaa kwa ajili ya michezo ya hatua za awali ya michuano ya @thebal inayotarajiwa kuchezwa Dar es Salaam kuanzia Oktoba 17-21, 2023.

Hasheem amesema, “sio mimi pekee ni timu ya Pazi kwa ujumla, wategemee mabadiliko katika basketball, kwa miaka mingi tunashiriki tu basi.

"Ila naona kama hatufiki ila muda wangu ukikaribia kabisa mimi kumaliza basketball pia unakaribia, lengo langu kubwa mimi kurudi nyumbani kuja kufanya basketball katika level ambayo Tanzania inatakiwa icheze,” amesems Hasheem.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live