Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Fainali NBA Dallas yaepuka ufagio

Dallas Mv Fainali NBA Dallas yaepuka ufagio

Sun, 16 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ushindi wa Vikapu wa vikapu 122-84 iliyoupata Dallas Mavericks jana Jumamosi asubuhi dhidi ya Boston Celtics, uliiepusha na aibu ya kupoteza mechi (series) za fainali saba za NBA kwa mechi nne (ufagio) baada ya kupoteza tatu za kwanza za fainali hiyo.

Dallas ikicheza kwa kutambua, ni aibu kupigwa ufagio kwenye fainali inayotokea mara chache baada ya miaka kadhaa, ilicheza ikisaka ushindi wa mapema baada ya kuongoza robo zote nne za mchezo huo uwanjani American airlines Center, Ukanda wa Magharibi.

Luka Doncic aliyecheza mchezo wote wa jana baada ya mchezo wa tatu kutolewa robo ya nne kutokana na kucheza faulo nyingi, alifunga pointi 29 na kulinganisha asisti na ribaundi tano wakati Kyrie Irving akifunga pointi 21, na ndio waliofunga zaidi ya pointi 20 kwenye mchezo huo.

Celtics ilitepeta kwenye mchezo huo na nyota wake Jayson Tatum alifunga pointi 15 pekee na ndiye aliyeongoza kwani Jaylen Brown aliishia pointi 10 tu kwenye mchezo huo waliozidiwa pointi 38 ikiwa ni tofauti kubwa kwao kupoteza msimu huu.

HIZI ZILIKULA UFAGIO

Mchezo wa jana, Dallas ilikuwa na uwezekano wa kuingia kwenye orodha ya timu tisa zilizowahi kupoteza fainali ya NBA kwa kuchapwa ufagio (sweep).

Kitendo cha Dallas kukwepa aibu hiyo ni kama kuibeba kanda nzima ya Magharibi na timu zake ndizo kinara kwa kuzichapa ufagio timu za Ukanda wa Mashariki, kwani mara tatu zote za mwisho kutokea hivyo, ni timu za Mashariki zilizokutana na kichapo hicho cha aibu.

Mwaka 2002, Brooklyn Nets ya Mashariki ilikula ufagio kutoka kwa Los Angeles Lakers ya Magharibi kwenye fainali ya NBA, wakati huo timu ikiwa na Kobe Bryant na Shaquille O’Neal na wengineo, timu iliyofuata baada ya hapo ni miaka mitano baadaye, Clevaland Cavaliers.

Cavaliers ilikula kichapo hicho mwaka 2007 kutoka kwa San Antonio Spurs ya Magharibi, kabla ya kusubiri tena miaka 11 kuja kupokea kichapo cha aina hiyo, kutoka kwa Golden State Warriors ya Magharibi.

Ndio, Cavaliers ya LeBron James ilikutana na kichapo hicho cha aibu mwaka 2018 kwenye fainali ya NBA, shughuli nzima ikiongozwa na Kevin Durant na Steph Curry ambao waliitawala vilivyo timu hiyo kabla ya LeBron James kuondoka na kwenda kujiunga na Los Angeles Lakers.

HISTORIA INAIPA TAJI CELTICS

Hadi sasa, katika historia ya NBA, hakuna timu iliyowahi kushinda series ya mechi saba baada ya kuwa nyuma kwa matokeo ya 3-0, kama ilivyo kwa Dallas na inataka kupindua matokeo na kuwa timu ya kwnza kufanya hivyo hasa mechi za fainali ambazo ni ngumu.

Mwaka 2016 Cavaliers ilishtua wengi ilipokuwa bingwa wa NBA mbele ya Golden State Warriors baada ya kutokea kufungwa 3-1 na kushinda 3-4 baada ya mechi saba, lakini hiyo ni tofauti na matokeo kuwa 3-0, haijawahi kutokea kwenye historia ya NBA hasa fainali.

LUKA AGOMA KUKUBALI

Luka Doncic wa Dallas anaamini baada tu ya kushinda mchezo wa nne, hakuna kitu kisichowezekana na wamejiandaa kwenda kushinda mchezo wa Jumatatu ugenini Uwanja wa TD Garden ili warudi nyumbani kwao kusawazisha matokeo yawe 3-3 na mchezo wa saba uwe wa kuamua mbabe.

Kauli ya Luka Magic ni kama iijibiwa na Jayson Tatum wa Celtics ambaye baada ya mchezo huo waliopoteza, alisema ni furaha kwake kupata fursa ya kwenda kushinda ubingwa huo uwanja wa nyumbani (TD Garden) na kuweka rekodi mpya ya kubeba taji la 18 ikiipiku Los Angeles Lakers.

MVP HUYU HAPA

Kabbla ya mchezo wa tano wa fainali, nyota anayeongoza kwenye vita ya kuwa kuwania mchezaji bora wa fainali (MVP) ni Jaylen Brown wa Celtics na ameibuka nyota wa mchezo kwenye mechi tatu za kwanza.

Kama Celtics itashinda mchezo ujao, bila shaka ndiye anatarajiwa kutangazwa MVP wa fainali huku kwa nyuma yake, akifuatiwa na Jayson Tatum.

Chanzo: Mwanaspoti