Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Doc Rivers apewa jukumu NBA

Documentary Doc Rivers

Fri, 26 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Kikapu ya Milwaukee Bucks inayoshiriki Ligi ya NBA (Eastern Conference) wamemuajiri Kocha wa zamani wa Los Angeles Clippers, Doc Rivers ili kuinoa timu hiyo kuchukua nafasi ya Adrian Griffin waliyeacha kufanya nae kazi

Milwaukee Bucks jukumu kubwa walilompa Kocha huyo mpya ni kuhakikisha anawapa Ubingwa wa Ligi hiyo kwani wanataka ubingwa wa pili ndani ya misimu minne (4) na mpaka sasa timu hiyo inashika nafasi ya pili (2) kwenye msimamo wa Eastern Conference nyuma ya Boston Celtics wakiwa na rekodi ya 30-13

Mara ya mwisho kwa Kocha Doc Rivers kuchukua ubingwa ni alivyokuwa na Boston Celtics mwaka 2008 na tangu aondoke Boston Celtics mwaka 2013 hajawahi kuchukua ubingwa wa NBA.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live