Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Denver Nuggets Mabingwa NBA Western Conference

Nuggets.jpeg Denver Nuggets Mabingwa NBA Western Conference

Wed, 24 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Denver Nuggets imeingia Fainali za Ligi ya mpira wa Kikapu Marekani (NBA) kwa mara ya kwanza katika historia yao baada ya ushindi wa pointi 113-111 dhidi ya Los Angeles Lakers kwenye Fainali ya Western Conference Alfajiri ya jana.

Pongezi kwa Nikola Jokic aliyefunga pointi 30, rebounds 14 na assists 13 na kuivusha Denver Nuggets kwa ushindi wa jumla ya Series 4-0.

Mfungaji Bora wa muda wote wa NBA, LeBron James akiwa katika mechi ya mwisho msimu wake wa 20 kwenye histora yake ya NBA amejiwekea rekodi binafsi kwa kufunga pointi 31 kwenye first half ya Game 4.

Mwamba huyo mwenye umri wa miaka 38, James kwa ujumla amefunga pointi 40, rebounds 10, assists tisa ingawa haikumsaidia Mfungaji huyo Bora wa muda wote wa NBA kuinusuru Lakers na kipigo cha nne mfululizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live