Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Danki ya Lebron yamrudisha NBA

Dankiiiii Danki ya Lebron yamrudisha NBA

Tue, 20 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Uliitazama fainali ya mchezo wa kikapu kwenye michuano ya olimpiki pale Ufaransa? Kama ndio basi lazima ulikua mmoja wa waliofurahia kama sio kushangazwa na ile Danki (Dunk) ya kusisimua iliyomhusisha staa wa kikapu duniani, LeBron James.

Guerschon Yabusele, ndio aliyezua gumzo siku hiyo kwa kufunga kikapu kwa staili ya danki mbele ya LeBron na kuwa miongoni mwa wachezaji wachache sana kuwahi kufanya hivyo kwa miaka yote 21 ya kucheza kikapu na hususan Ligi ya Kikapu Marekani (NBA).

Ni danki Ile ambayo iliongeza thamani ya Yabusele ambaye hatimaye msimu ujao ataonekana kwenye ligi ya NBA akiwa na timu ya Philadelphia 7ers ya mkali Joel Embiid baada ya awali kuwahi kuchaguliwa kama namba 16 na Boston Celtics lakini hakufanikiwa kung'ara kwenye ligi na kuishia kucheza nje ya NBA ikiwemo nchini China.

Yabusele aliyekua anaitumikia timu ya kikapu ya Real Madrid ya Hispania, amepewa mwaka mmoja kuichezea Sixers na kupata fursa ya kuthibitisha uwezo wake aliouonesha kwenye olimpiki akifunga wastani wa pointi 14 kwa kila mchezo.

Chanzo: Mwanaspoti