Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Dallas waichungulia Fainali NBA, Boston yatangulia

Dallas Sss Dallas waichungulia Fainali NBA, Boston yatangulia

Fri, 31 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dallas Mavericks inahitaji kushinda mchezo mmoja pekee kati ya michezo mitatu iliyosalia ya fainali ya kanda ya magharibi (Kama kuna umuhimu), ili kucheza fainali kuu ya NBA msimu huu.

Hadi sasa Dallas Mavericks inaongoza kwa ‘Series’ ya 3-1 dhidi ya Minnesota Timberwolves na iwapo itashinda mchezo wa tano alfajiri ya kesho Ijumaa saa 9:30, itakuwa imefuzu kucheza fainali kuu ya NBA 2024.

Tayari kiulaini mabingwa mara 17 wa NBA Boston Celtics, mapema tu wametinga fainali kuu kufuatia ushindi wa ‘Series’ 4-0 dhidi ya Indiana Pacers, katika fainali ya kanda ya mashariki.

Iwapo Dallas Mavericks itafuzu kucheza fainali ya NBA msimu huu itakuwa kwa mara ya kwanza tangu washinde taji hilo 2011, wakati kwa Boston Celtics yenyewe imejihakikishia kulifukuzia taji la 18 la NBA ili kuwapiku wapinzani wao Los Angeles Lakers ambao wote wameshinda mara 17.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live