Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

CHRIS PAUL: Staa wa NBA anayestaafu kibosi

Paul Pic Data Chris Paul

Tue, 5 Jul 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Ukiangalia bili ya mshahara ya wachezaji wa timu ya Phoenix Suns inayoshiriki Ligi ya Kikapu ya Marekani, NBA, mchezaji anayeongoza kwa kuchukua mpunga mrefu ni Chris Paul ambaye anapata jumla ya Dola 38 milioni kwa mwaka.

Umri wake kwa sasa ni miaka 35 na hana muda mrefu sana kabla hajastaafu lakini anakwenda kupumzika akiwa na kitita cha kutosha kwenye akaunti yake ya benki sambamba na vitega uchumi vingine. Mwanaspoti hapa inakuonyesha jinsi jamaa anavyoenda kustaafu kibosi.

ANAPIGAJE PESA

Kwa mujibu wa jarida la Forbes jamaa anashika namba 31 kwa kuwa mwana michezo mwenye mpunga mrefu zaidi duniani hadi kufikia mwaka 2021, lakini alishika nafasi ya pili kwenye msimu uliopita wa NBA kwa kuwa mchezaji aliyevuna pesa nyingi zaidi akikunja Dola 40 milioni.

Mbali ya mshahara ambao kwa mwaka huvuka zaidi ya Dola 40 milioni, Paul anavuta mkwanja mwingine kupitia madili yake nje ya uwanja ambapo kwa ujumla anapata Dola 8 milioni kutokana na ubalozi wake wa kampuni za Panini, Nike, Air Jordan, Tissot na State Farm.

Mbali ya ubalozi wake wa kampuni mbali mbali kuna mpunga mwingine anaupata kupitia uwekezaji mkubwa alioufanya kwa kampuni kama Hyperice ambapo amewekeza zaidi ya Dola 48 milioni, Chirpify RSPCT Basketball na Beyond Meat

MIJENGO

Anamiliki mijengo miwili wakwanza ni ule uliopo Encino, California nchini Marekani ambao una thamani ya Dola 11.1 milioni. Hapa amejenga nyumba mbili sehemu moja ambazo zipo ndani ya uzio mmoja, hivyo nyumba moja anaitumia kwa ajili ya wageni na nyingine ni kwa ajili yake mwenyewe. Nyumba zote zimepambwa na vivutio kibao ndani yake ikiwa pamoja na mabwawa ya kuogelea na viwanja vya kuchezea michezo mbali mbali.

Nyumba nyingine alikuwa nayo huko Woodland Hills, Los Angels lakini aliiuza kwa Dola 1.95 milioni wakati anahama Jijini humo.

MAGARI

Jamaa ana ndinga kibao ikiwa pamoja na Jeep JKU Wrangler Unlimited, Range Rover na 1977 Chevrolet Monte Carlo.

MSAADA KWA JAMII

Amekuwa akionekana kwenye shughuli nyingi za kuchangia jamii miongoni mwa hizo ni ile kampeni ya After-School All-Stars ambayo ina lengo la kutoa msaada wa kipesa kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kulipa ada.

Pia amewahi kushiriki mara kadhaa kwenye kampeni kama Aid Still Required, Boys & Girls Clubs of America, Girl na Make It Right.

Kubwa zaidi anamiliki taasisi iitwayo CP3 Foundation yenye lengo kusaidia jamii.

MAISHA NA BATA

Yupo kwenye ndoa na mrembo Jada Crawley ambaye amezaa naye watoto wawili ambao mmoja ni wa kike na mwingine ni wa kiume.

Chanzo: Mwanaspoti