Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Brittney Griner: Mahusiano ya jinsia moja na shutuma anazokumbana nazo

Brittney Griner 0a4ab26 Brittney Griner

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Huenda muonekano wa mwili wake ulimshawishi zaidi kupenda mchezo wa kikapu (basketball). Brittney Grinner ni mwanamke na mchezaji mahiri wa mchezo pendwa wa kikapu Marekani, upande wa wanawake.

Katika orodha ya wachezaji bora ishirini na tano (25) waliotajwa mwaka 2023 Brittney yupo nafasi ya kumi na tatu. Anachezea timu ya Phoenix Mercury. Amewahi kushinda medali mbili (2) za dhahabu katika michezo ya Olympic alipokuwa anawakilisha timu ya taifa ya wanawake katika mchezo huo wa kikapu. Pia mwaka 2023 katika gazeti maarufu la Times alitajwa kama mmoja wa watu 100 wenye ushawishi zaidi duniani.

BRITTNEY NA ‘MKE WAKE’ CHARELLE WANATARAJIA MTOTO

Usichojua kuhusu Brittney ameoa na yeye na mkewe wanatarajia mtoto. Katika habari zilizogusa mitandao ya kijamii ni pamoja ya hii ya wawili hawa kutarajia kupata mtoto. Jumamosi ya tarehe 15 Aprili, nyota huyo wa mpira wa kikapu aliweka picha ya mkono wake na ‘mpenzi’ wake Cherelle na ujumbe “Siamini kama tuna miezi mitatu pekee ya kukutana na mpendwa wetu”. Mtoto ambae amepatikana kwa njia ya upandikizaji.

Watu wengi wamekuwa na maoni tofauti juu ya mahusiano hayo ambayo kiuhalisia yanapingana na tamaduni, mila,desturi na hata imani za kidini. Katika mitandao ya kijamii kumekuwa na maoni mbalimbali juu ya uhusiano wao na wengi wakiwaandikia maneno kama ‘wenye dhambi’, ‘ndoa pekee ni ya mwanamke na mwanaume’.

Hii si ‘ndoa’ yake ya kwanza aliwahi pia ‘kuoa’ 2015 na alimuoa mchezaji wa kikapu aliyefahamika kama Glory Johnson na inasemekana walipata watoto mapacha wawili. Mwezi mmoja baada ya ndoa yao Brittney alifungua mashtaka kwamba ndoa hiyo haikuwa sahihi kisheria na alilazimishwa lakini mahakama ilikataa pingamizi hilo na kumuamuru kutoa matumizi ya mtoto. Baadae 2016 talaka rasmi ilitoka.

Brittney aliwahi kukamatwa huko nchini Russia na kukaa kizuizini kwa siku 3oo kabla ya kuhukumiwa miaka tisa (9) jela. Inadaiwa alikutwa na dawa za kulevya ambapo baadae ilidaiwa alikamatwa kimakosa na kuachiwa huru.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live