Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Aziz KI sio soka tu, mwamba anakiwasha mpaka basketball

Aziz Ki Baskett Aziz KI sio soka tu, mwamba anakiwasha mpaka basketball

Thu, 30 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/23, Stephanie Aziz KI licha ya kupewa mapumziko, jana alionekana akifanya mazoezi a timu ya mpira wa kikapu ya Dar City huku akisema kwamba mchezo wa kikapu ndiyo mchezo wake pendwa namba moja kisha soka, lakini amewekeza nguvu na jitihada kubwa kwenye mpira wa miguu.

Aziz KI ambaye ni raia wa Burkina Faso ameonekana muda mwingi akihudhuria mechi za mpira wa kikapu lakini mara hii ameonekana akicheza mwenyewe dimbani na kutupia mabao ya kutosha wakati timu hiyo ikijiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi ya Kikapu nchini.

“Mungu ndiye amenipa vipaji hivi, hapa nimekuja kuipa sapoti Dar City kwa sababu Rais wake (Ally Mzenji) amekuwa akija kwenye mechi za Yanga hata Afrika Kusini alikuja kutusapoti, kwa hiyo ni jambo la mhimu kwangu kuja hapa kufanya nao mazoezi na kuwapa moyo.

“Nimewahi kucheza basketball lakini kwa sasa ninajifurahisha tu. Baskrt ndiyo mchezo wangu pendwa namba moja kabla ya soka, lakini kwa sasa sina ndoto tena ya kucheza basket baadaye kwenye maisha yangu bali kujifurahisha tu. Basket ninajaribu si kwamba niko vizuri sana.

“Basket inahitaji nguvu zaidi kuliko football, kwangu ni jambo jema kuja kucheza na kupata fitness kwa sababu nina mechi ya fainali dhidi ya Azam FC. Kwa hiyo ni sehemu ya mazoezi kwangu kuelekea fainali,” amesema Aziz KI.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live