Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MenuMichezo
Mpira wa Kikapu

Atolewa figo baada ya kuumia mchezoni

Bogdan Bogdanovic FIBA World Cup Borisa Simanic.jpeg Atolewa figo baada ya kuumia mchezoni

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa Mpira wa Kikapu wa Serbia Borissa Simanic, amelazimika kutolewa figo baada ya kujeruhiwa wakati wa mechi ya Kombe la Dunia huko Philippines.

Simanic alipigwa tumboni na mchezaji kutokea Sudan Kusini Nuni Omot wakati wa mechi yao iliyochezwa Jumatano iliyopita.

Alifanyiwa upasuaji siku hiyo hiyo jijini Manila lakini kutokana na matatizo kujitokeza upasuaji mwingine ulifanywa Jumapili ya juzi ndipo figo ilipotolewa.

Maafisa wa mechi husika wamesema tukio la uwanjani lilikuwa la bahati mbaya na Omot ameomba radhi.

"Nimesikitishwa sana na kilichotokea, nikiwa kama mwanamichezo ninaelewa uzito wa hili, ninaomba radhi sana"

"Hakuna mchezaji anayestahili kupitia jambo kama hili, namuombea Simanic apone haraka na aweze kurudi uwanjani" alisema Omot.

Michuano ya FIBA Basketball World Cup ilianza Agosti 25 na inatarajia kumalizika Septemba 10. Wenyeji wa michuano hiyo ni Indonesia, Japan na Philippines.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live