Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wiz Khalifa auza haki ya nyimbo zake

IMG 4580.jpeg Wiz Khalifa

Sun, 9 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wiz Khalifa ameungana kwenye kambi ya wasanii wa Hip Hop ambao hivi karibuni wameuza haki ya baadhi ya nyimbo zao ‘Catalogs’ kwa Makampuni. Juzi Alhamis (July 6), Kampuni kubwa ya uwekezaji duniani HarbourView Equity waliingia dili na Wiz na kuwauzia sehemu ya nyimbo zake.

Makubaliano yao ambayo hayataja kiasi hadharani, yamejumuisha Album kadhaa za Wiz Khalifa pamoja na Mixtapes na Singles ambazo zimemtambulisha hadi leo ikiwemo; Black & Yellow, See You Again, The Thrill na nyingine kibao.

Wiki hii pia Nelly alitangaza pia kuuza sehemu ya nyimbo zake kwa Kampuni hiyo kwa kiasi cha ($50 million) zaidi ya TSh. BILIONI 122, ikijumuisha Album Nane za mkali huyo wa R&B na Hip Hop.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live