Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Video zinakomba pesa za wasanii - Alikiba

Alikiba Hnnnn Alikiba

Wed, 29 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa mziki nchini Alikiba amesema video zinamaliza pesa nyingi kwa wasanii tofauti na audio ambazo zinaingiza pesa bila shida yoyote.

Akizungumza nasi #AliKiba anasema; "Ni kweli tunafanya video lakini ukweli video inachukua pesa nyingi sana kwa wasanii na wanasubiri pesa zirudi.

"Unajua mziki ni biashara maono yangu nimejaribu kufanya mwaka huu '#LyricsVideo' ili waone reaction yangu nilivyoimba na kudeliver mziki wangu kupitia lyrics or dancing video.

"Wasanii wamekuwa wakipoteza pesa bila kujijua hiyo tafiti nimeifanya baada ya kutoa 'The Only One King' kuna video ambazo zimeingiza pesa zingine hazikuingiza pesa lakini audio ina penetrate na kuingiza pesa bila shida yoyote," amesema Kiba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live