Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tamasha la Jay Z lasitishwa

Jigga Jay Z Jay Z

Thu, 10 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tamasha la Made In America linalofanywa kila mwaka na nyota wa muziki Jay-Z lililotarajiwa kufanyika mwezi ujao Philadelphia limeghairishwa hadi mwaka ujao.

Kughairishwa kwa tamasha hilo kumeonekana kuwaumiza mashabiki waliotegemea kufurahi na Jay Z pamoja na wasanii wengine waliokuwa wametarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo.

Tamasha hilo lilitarajiwa kuanza Septemba 2-3 Philadelphia, lakini hadi sasa bado hazijatajwa sababu maalum za kughairishwa kwake.

Kila mwaka tamasha hilo limekuwa likifanyika tangu mwaka 2012, isipokuwa mwaka 2020 lilishindikana kutokana na janga la COVID-19.

Kati ya wasanii waliokuwa wakitarajiwa kuimba siku hiyo ni Miguel, Tems, Metro Boomin, Ice Spice, Coi Leray, Latto, Lil Yachty, Doechii, Lola, na wengine wengi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live