Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

R Kelly: Nakiona kifo kiko mbele yangu

 125678053 Kelly R Kelly

Fri, 23 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Muziki kutoka Marekani Robert Kelly (R. Kelly) amemwaga machozi akiwa Gerezani, kwenye sauti iliyodakwa na #RaphouseTv ameweka wazi Kwamba hapati huduma bora Gerezani ikiwa ni baada ya kubainika ana tatizo la damu kuganda lililopelekea kuwa na hofu ya maisha yake Gerezani.

R Kelly amesikika akisema kwamba; "Nina hofu na maisha yangu, kwani sipaswi kufa kwa sababu ya chuki ya mtu ambaye hajali tatizo la mguu wangu.

"Vipi angekuwa baba yako, mama yako, mtoto wako au mtu umpendaye angepatwa na tatizo hili (ungeshauri aende akapatiwe matibabu na Daktari), lakini kwangu haikuwa hivyo.

"Hata X-Ray hamjanifanyia. Ninahofia maisha yangu katika eneo hili, ilikuwa karibu nife, kwani hata wanyama wanapewa huduma Bora kuliko mimi," alisema Kelly.

R Kelly kwa Sasa anatumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa makosa ya unyanyasaji wa kingono.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live