Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pindi Chana: BASATA hawakimbilii kufungia wasanii

Pindi Chana Bungeni.jpeg Balozi Dkt. Pindi Chana

Tue, 6 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana leo amewasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka 2023/24 Bungeni Dodoma ambapo moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba yake ni kwamba BASATA kwa sasa imeendelea kutokimbilia kuwafungia Wasanii kama ilivyokuwa awali.

“Serikali kupitia BASATA imeendelea kukuza ubunifu na utengenezaji wa sanaa bora kwa lengo la kuwawezesha Wasanii kuwa Wabunifu na kubuni kazi za sanaa zilizo bora, BASATA liliendelea na mageuzi ya kiutendaji na kitaasisi ili kuwa mwezeshaji zaidi wa shughuli za sanaa badala ya kudhibiti”

“Hivyo, BASATA limeshiriki kuratibu kutatua migogoro ya wasanii kuhusu mikataba waliyoingia ambapo katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Aprili, 2023 zaidi ya migogoro mikubwa mitano imetatuliwa, BASATA pi alimekuwa likiwaita Wasanii sio tu pale kwenye upungufu bali hata pale wanapofanya vizuri na kuwapongeza”

“Sambamba na hatua hii, BASATA limeendelea kutokimbilia kuwafungia Wasanii kama ilivyokuwa awali bali kunapotokea changamoto zilizokithiri za kimaadili, kama alivyoagiza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wakati wa Tamasha la Usiku wa Msanii Joseph Mbilinyi”

“BASATA limeendelea kutoa Tuzo za Muziki wa Tanzania (TMA) kwa mara ya pili mfululizo, Tamasha la utoaji wa Tuzo hizi lilifanyika Dar es Salaam April 29, 2023, ukihusisha utoaji wa Tuzo maalumu zilizotolewa kwa Taasisi Nne ambazo ni UDSM, Chuo cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, Clouds Media Group na Sauti za Busara, Zanzibar”.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: