Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nyota wa Reggae afariki Dunia, aacha watoto 41

Aston Familyman Barrett Nyota maarufu wa Muziki wa Reggae Aston Barrett

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota maarufu wa Muziki wa Reggae Aston Barrett( 77) wa Jamaica, amefariki dunia.

Barrett alianza kupata umaarufu akiwa kwenye Bendi ya Upsetters, iliyokuwa chini ya Mwanzilishi mmojawapo wa Reggae Lee ‘Scratch’ Perry. Mwaka 1974 alijiunga na bendi ya Bob Marley.

Barrett almaarufu kama “Family Man”alikuwa mpiga besi (bassist) wa bendi ya Bob Marley and the Wailers, na alikuwa mmoja wa watu waliochangia sana kukua kwa Reggae.

Mwanamuziki huyo Mkongwe alikuwepo karibia katika kila album ya Wailers, pamoja na kufanya kazi na wanamuziki maarufu kama Burning Spears, Peter Tosh na wengine wengi.

Baadhi ya vibao maarufu ambavyo alikuwemo ni pamoja na ”Get up Stand Up, Stir It Up, No Woman, No Cry na Could You Be Love”.

Kupitia mtandao wa Instagram, Mtoto wa Mwanamuziki huyo Aston Barrett Junior alisema “ Kwa mioyo mizito, tunatoa taarifa za kifo cha mpendwa wetu Aston ‘Familyman’ Barrett, baada ya vita vya muda mrefu vya matibabu”.

Katika mahojiano yake na BBC yaliyofanyika mwaka 2013, Barrett alisema kuwa ana watoto 23 wa kike na 18 wa kiume, mimi ni “mwanaume wa familia/ family man, nimejaliwa watoto 41”.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live