Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Nikki: Muziki bado pasua kichwa

Niki Mbishi Nikki: Muziki bado pasua kichwa

Fri, 9 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MSANII wa HipHop, Nicas Mchuche’Nikki Mbishi ‘amesema haamini kwenye mauzo ya muziki yanayofanyika kupitia majukwaa ya mitandao.

Mwanamuziki huyo amesema hiyo ndio sababu ya kuamua kusambaza albamu yake mpya ya katiba yeye mwenyewe.

Nikki anasema hafikirii kama Tanzania imesonga mbele kwenye suala la mauzo ya muziki mitandaoni kwani malipo yake yamekuwa hayatoi taswira njema akilinganisha na wakati ambao hakukuwa na mauzo ya mitandaoni.

“Huwezi kusema sasa hivi muziki unakuwa au unaenda mbele wakati zamani mtu hajamaliza kazi ashapewa fedha, lakini sikuhizi unamaliza kazi, unatoa albamu unaitangaza alafu unakuja kupewa milioni moja baada ya miezi minane” amesema Nikki

Nikki Mbishi anaendelea kuisambaza albamu yake mpya ya katiba aliyoiachia wiki nne zilizopita na ameamua kuiuza kupitia mitandao binafsi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live