Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Muziki haikuwa ndoto yangu - Aslay

Aslay  23 800x445.png Muziki haikuwa ndoto yangu - Aslay

Thu, 27 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii nguli wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka amesema kuwa hakuwahi kuwaza kuwa atakuja kuwa msanii mkubwa wa muziki kwani kipache chake akiwa mdogo ilikuwa ni kucheza soka na ndiyo yalikuwa malengo yake ya baadaye.

Aslay ambaye yupo kwenye game ya muziki mwaka wa 10 sasa anasema alishawishiwa na kaka yake kuingia kwenye muziki lakini haikuwa hobi yake kabisa tangu akiwa mdogo.

Tumsikie Aslay anasemaje; "Show ya mwisho nimefanya Nairobi Kenya hivi karibuni, kule Nairobi ni kama nyumbani walinipokea vizuri kwa sababu Nairobi wanapenda sana muziki wetu wa Tanzania wa Bongo Fleva.

"Nimetimiza miaka 10 kwenye muziki, na mwanzoni sikuwaza kabisa kuwa Mwanamuziki, nilikuwa napenda kucheza soka. Wakati naanza muziki kaka yangu mmoja ndiye aliyenisukuma niingie kwenye muziki.

"Mtaani kwetu tulikuwa tukikaa ulikuwa unamsikia Barnaba ameimba na wewe unamuiga, kaka yangu aliponisikia aliniona kama nina kitu, kwahiyo sikuwaza kama nitakuwa mwanamuziki na sikuwaza kama nitafika hii miaka 10, baadae niliona kumbe muziki ni sirious," amesema Aslay.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live