Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Drake ahusika kwenye albam ya baba yake

For All The Dogs Drake Mtoto wa Drake ahusika kwenye albam ya baba yake

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uhusiano wa supastaa wa muziki nchini Marekani, Aubrey Drake Graham 'Drake' na mtoto wake #Adonis ni mkubwa sana kiasi cha kwamba anaanza kumshirikisha kwenye kazi zake za muziki.

Drake ameweka wazi kuwa Adonis amehusika kuchora mchoro wa kava la Album yake ijayo #ForAllDogs inayotarajiwa kuachiwa Ijumaa hii Agosti 25, 2023.

Mchoro huo unaonekana kuwa wa mbuzi mwenye macho mekundu na masikio marefu na kiwiliwili cheupe.

Ni wiki chache zimepita Drizzy akiwa jukwaani hivi karibuni kwenye tour yake ya It's All a Blur, huku rapper huyo akikwepa mambo yaliyokuwa yakimrushiwa jukwaani na mashabiki ikiwa ni pamoja na sidiria na vapes kwenye simu za mkononi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live