Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mtoto wa Alicia Keys na Swizz Beatz hana mpango na muziki

Egypt Dean(33).jpeg Mtoto wa Alicia Keys na Swizz Beatz hana mpango na muziki

Sat, 10 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya wazazi wake kujihusisha na muziki hadi kuwa watu wenye nguvu ya ushawishi duniani, mtoto wa Alicia Keys na Swizz Beatz, Egypt Dean, 12, hana kabisa mpango wa kuja kuwa mwanamuzki siku za mbeleni.

Alicia na Swizz walifunga ndoa Julai 31, 2010 katika sherehe ya faragha iliyofanyika karibu na bahari ya Mediterania, Alicia, 42, alijifungua mtoto wao wa kwanza wa kiume, Egypt, Oktoba 2010 na wa pili, Genesis, Desemba 2014.

Egypt akiwa na baba yake, Swizz katika mahojiano na The Jennifer Hudson Show, alisema inafurahisha kwa sababu anapenda kucheza na vyombo vya muziki kama Piano ila ndoto yake sio kuja kuwa mwanamuziki.

"Sawa, napenda muziki, lakini sitaki kabisa kuwa mwanamuziki, nataka kuja kuwa mchezaji wa mpira wa kikapu. Inachekesha kwa sababu napenda kucheza vitu kama Piano, inanifurahisha sana ninapoisikia," amesema Egypt.

Utakumbuka Swizz Beatz ni Prodyuza wa Marekani na ametengeneza nyimbo maarufu kama; Jigga My Nigga, Girl's Best Friend za Jay Z, Upgrade U, Chek on It, Ring the Alarm za Beyonce, Touch IT ya Busta Rhymes na Ultralight Beam ya Kanye West n.k.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live