Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mpiga kinubi namba moja duniani kutumbuiza Mlima Kilimanjaro

Mpiga Kinubi Mlima Kilimanjaro.png Mpiga kinubi namba moja duniani kutumbuiza Mlima Kilimanjaro

Thu, 20 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki na mpiga kinubi maarufu aliyeshinda tuzo za Guiness kwa kufanya onesho katika kilele cha mlima Kilimanjaro, Siobhan Brady amewasili nchini Julai 19, 2023 kwa ajili ya kuvunja na kuweka rekodi mpya katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.

Msanii huyo ambaye onesho lake la kwanza alilifanya Septemba 2018 kwenye kilele cha Mlima Singla, Himalaya nchini India wenye urefu wa mita 4,954 kutoka usawa wa bahari.

Huu ni mkakati wake wa kuvunja rekodi yake hiyo na kuweka mpya kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu kuliko yote barani afrika ukiwa na urefu wa mita 5,895 kutoka usawa wa bahari.

Brady ambaye ameambatana na baba yake, Sean Pamoja na kundi lake lijulikanalo kama Highest Harp amesema amekusudia kufanya onesho hilo ili kusaidia wale wenye matatizo ya uvimbe tumboni (Cystic Fibrosis) nchini Ireland.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live