Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Morgan Heritage kuachia albam mpya

Morgan Heritage Rg.png Kundi la Morgan Heritage

Fri, 24 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kundi la Morgan Heritage lafunguka kuwa soon litaachia Album yao inayoenda kwa jina la “Homeland” Aprili 21, 2023 na ambayo wamejumuisha Wasanii mbalimbali wa Africa pamoja na Marekani.

Hii ni baada ya kuachia ngoma mpya tokea Januari mwaka huu, kwenye hii album ambayo ni ya aina ya Afro Fusion, pia kutakuwa na Rj the Dj pamoja na Eddy Kenzo, Jose Chameleon toka Uganda na usisahau pia wamemjumuisha Otile Brown wa Kenya.

Hawa ni baadhi tu ya wasanii waliotajwa mbali na Shaggy, Youssou, Popcaan, Beenie Man, Shatta Wale, Busy Signal, Alpha Blondy, Made Kuti, Carleton, Ice Queen Cleo, Macky 2 na wengine tokea Carribean na Africa.

Kwa sasa wimbo wao mpya amabayo unatesa kwenye media zetu ni ‘Who De Like You’ ambao waweza usikiliza katika mitandao iliyopakiwa hapa nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live