Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mkongomani aifuta Enjoy ya Jux na Diamond huko YouTube

Diamond Jux Cds Enjoy ya Jux na Diamond yafutwa YouTube

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii kutoka Congo anayefahamika kwa jina la Issas Joana (22), maarufu kama Sapologuano Odenumz, ameifuta audio ya Enjoy ya Juma Jux ambayo amemshirikisha staa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.



Sapologuano amedai kuwa ameufuta wimbo huo kwa sababu wame-copy ngoma yake yake ya 'I found Love'.

Msanii huyo ameenda mbali zaidi na kueleza kuwa iwapo hawatamalizana naye ndani ya siku mbili basi wajiandae kwa pigo jingine takatifu kwani ataifuta hata video ya wimbo huo.

Akihojiwa kuhusu uamuzi wake huo, Sapologuano ameweka wazi kuwa siku kadhaa nyuma aliwahi kumtumia Jux ili wafanye kazi lakini msanii huyo alimzungusha na amekuja kuisikia Melody yake kwenye wimbo wa Jux na Diamond #Enjoy.

Aidha, Sapologuano ameongeza kuwa hivi karibuni alimtafuta Jux ili wazungumze na waone namna ya kulimaliza suala hilo lakini staa huyo wa Bongo Fleva alimkaushia jambo lililomfanya kuamua kuifuta YouTube.

Nini maoni yako?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live