Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mistari ya Roma inavyotikisa mitandaoni - Video

Video Archive
Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa kutokea nchini Tanzania ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani, Roma Mkatoliki ameachia wimbo mpya unaoenda kwa jina la “Nipeni Maua Yangu” ambao hakika umekuwa gumzo mtandaoni kupitia aina ya mashairi aliyoweka katika wimbo huo.

Baada ya wimbo huo ku-trend sana na kuwafikia watu wengi, wamekuwa na maoni na mitazamo tofauti ya kusema kuhusiana na mashairi ya wimbo huo.

Baadhi ya Viongozi wa Kisiasa wamemshauri Msanii huyo aweze kurejea nchini kwake kwa kumtoa hofu kuwa hali ni nzuri chini ya Uongozi wa awamu ya 6 nchini Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan

Hizi ni niongoni mwa tungo za mashairi yanayopatikana katika wimbo wake mpya #NipeniMauaYangu

“Tatizo mkishaapishwa tuu mnawaza uchaguzi ujao,hamuwazi njia mbadala ya kumlinda mkulima na mazao sasa Iringa si kuna msitu halafu Toothpick tunaagiza China make kwanza hapo nicheke,” amesema Roma Mkatoliki.

“Mimi sio CCM wala CHADEMA, simwamini mtawala na mpinzani simsadiki, maana wanaendelea kukatika huku DJ kauzima mziki,” amesema Roma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live