Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kusah: Siwezi kufanya Amapiano

Kusah Ms Msanii Kusah.

Thu, 27 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Salmin Ismail Hoza maarufu kama Kusah amesema kuwa yeye hawezi kufanya muziki wa Amapiano licha ya mastaa wengi kukumbwa na omwe la kufanya muziki huo ambao asili yake ni Afrika Kusini.

Kusah amesema Amapiano sio hobi yake na haamini kama anaweza kufiti kufanya aina hiyo ya muziki ambayo ndio trending kwa Bongo sasa hivi.

Ikumbukwe kuwa mastaa kama Diamond Platnumz, Alikiba, Harmonize, Rayvanny, Marioo, Zuchu na wengine wengi wameshafanya ngoma kibao za Amapiano ambazo zimepokelewa vizuri na mashabiki na zinakimbiza huko mitandaoni.

“Amapiano ni muziki mzuri umepokelewa ila mimi sina hobi nao, nilijaribu kufanya fanya hapo nyuma lakini sikuwahi kutoa ila nikaona kabisa siwezi ku-fit!

"Unajua sio kufanya kitu kwa sababu kina Marioo wamefanya, kikubwa ni kufanya vitu vya tofauti ambavyo wengi hawajavifanya na kufika hapa walipofika leo, sio lazima nifanye Amapiano!”

“Naamini kila mtu ana nafasi yake, si unaona nimetoa ngoma ya Mungu na inafanya poa iko namba moja Tiktok, naamini ukiwa mbunifu huwezi game haiwezi kukuacha,” amesema Kusah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live