Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Konde Boy atangaza vita...

Harmonize+pic Konde Boy atangaza vita...

Fri, 9 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Bongo flavor, Rajabu Abduli Kahali 'Harmonize' ametangaza kupitia instagram stori yake kuwa mwanamuziki yeyote anayejiamini nchini washindane kutumbuiza ana kwa ana katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar-es-salaam.

"Huku nikifikiri kwa sauti, nahitaji nishindane kutumbuiza na msanii yeyote mnayemuaminia kwa kutumia vyombo (music band), isiwe wimbo wa kushirikishwa wala kushirikiana. Tukutane Benjamin Mkapa."

Katika andiko lake hilo Harmonize ameongeza kuwa ili kushindana msanii huyo anapaswa kuwa na nyimbo zisizopungua 100.

Na kuhitimisha "Asiyeshindikana, niite namba moja (1), Kondeboy."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live