Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Harmonize apigwa na kitu kizito kichwani

Harmonize Country Harmonize apigwa na kitu kizito kichwani

Thu, 8 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Country Boy, msanii ambaye kwa wakati mmoja alikuwa katika lebo ya Harmonize, Konde Music Worldwide ameibuka upya na kufichua kwamba ameanzisha lebo yake na tayari amewapa mkataba wasanii watatu kwa mpigo, kwa jina Freshi Boys.

Msanii huyo ambaye aliondoka Konde kwa njia ya kishari baada ya kudai kukatishwa kwa mkataba wake alikanusha maneno ya walimwengu kwamba hawezi kuendesha lebo kwa sababu hana hela, na ili kufanikisha kuendesha lebo basi sharti amfuate aliyekuwa bosi wake Harmonize ili kumuomba msaada.

Country alisema kuwa hana mawasiliano na Harmonize na wala hana ushikaji naye huku akisisitiza kwamba msanii huyo wa Aiyola hakuwahi kuwa na umuhimu wowote kwa upande wake tangia kipindi alipokuwa pale na hata alipotoka.

“Haiwezekani kwa sababu hata hatuongei. Hainigharimu kitu chochote kwa sababu alikuwa mwanangu, lakini ule ushikamano ulishapotea kitambo na kila mtu anaendelea na maisha yake. Na siamini kwamba yeye ana umuhimu kwenye upande wangu ndio na hata mimi sina, ndio maana hata nilivyotoka hakuumia, anaendelea na maisha yake,” Country Boy alisema.

Msanii huyo pia alifutilia mbali uwezekano wake kufanya collabo na Harmonize akisema kuwa pengine anaweza akawa na umuhimu kama msanii na kuwapa vesi wasanii wake Freshi Boys.

“Anaweza akawa na umuhimu kama msanii mwenzangu ambaye anaweza akasapoti, afanye nao ngoma. Mimi nadhani anaweza akawapa hata collabo Freshi Boys kwa sababu ni vijana wenye talanta,” alisema.

Msanii huyo ambaye sasa ameshakuwa mkurugenzi wa lebo alisema kuwa wengi wanamchukulia kuwa hana hela kwa kufngua lebo lakini akasema amewashika vijana mkono na amaamini ni watu ambao wanategemewa na familia vile vile.

“Mashabiki wanaamini kwamba rekodi lebo ni kuuza mandazi, kusajili kampuni ni hela. Kwa hiyo sijapoteza muda wangu, nimewekeza. Japo ni kidogo na ni kweli mimi sina hela kweli lakini nina hela ya kumfanya kila mtu akala,” alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live