Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Franco Luambo atakumbukwa

Franco Luambo Franco Luambo.

Thu, 3 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mpiga gitaa wa Jazz wa Kongo Franco Makiadi alipofariki mwaka 1989, Zaire nzima iliingia katika maombolezo makubwa kumuaga kwa huzuni mwanamuziki ambaye, kwa muda wa miaka 40, alitoa zaidi ya albamu 150, zenye nyimbo zaidi ya 1000, na ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa katika muziki wa Kiafrika.

Franco ambaye alizaliwa Tarehe 6 Julai, 1938, katika Kijiji cha Sona Bata Magharibi ya Kongo, atakumbukwa na watanzania wakati alipofanya onyesho kweye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwaka 1973.

Franco alipofikisha umri wa miaka Saba alitengeneza gitaa la kienyeji ambalo alilitumia kupiga na akiwavutia wateja pembeni mwa mama yake wakati akiuza mikate.

Mwaka 1950, wakati huo akiwa na umri wa miaka 12, alitengeneza jina akiwa katika bendi ya Watam ya Ebengo Dewayon ambaye alikuwa kiongozi wa bendi hiyo.

Alizikonga nyoyo za wapenzi kwa uwezo wakemkubwa wa kupiga gita ambalo lilikuwa kubwa kuliko yeye.Miaka mitatu baadaye Franco alirekodi wimbo wake wa kwanza uliokuwa na jina la Bolingo na Ngai na Beatrice. Baadaye kukubalika kuwa mmoja wa wana bendi ya Loningisa Studio.

Mwaka 1955 Franco aliunda bendi akiwa na Jean Serge Essous iliyokuwa ikipigia katika Baa ya Ok huko Kinshasa.

Mwaka uliofuatia bendi hiyo ilibadilishwa jina na kuwa Ok Jazz na baadaye ikaitwa T.P.Ok. Jazz kuenzi sehemu ilipoanzia bendi hiyo yaani katika Bar yenye jila la OK (OK. Bar)

Katika kipindi cha mwaka mmoja bendi yake ya T.P.Ok Jazz ikagundulika kwamba inataka kumpiku Vicky Longomba ambaye alikuwa katika bendi ya Grand Kale ya African Jazz ambayo ndiyo ilikuwa bendi kubwa nchini Kongo.

Ok Jazz iliisaidia sana Serikali ya Mobutu katika mambo ya kisiasa. "Umesikia jinsi anavyokuongelea vibaya kwa watu Mario", hayo ni maneno ya Franco Luambo kwenye wimbo wake wa Mario. Mario kilikuwa ni kisa cha kweli mwanaume msomi aliyekuwa ana ishi na kulelewa na wanawake huko Ureno. kuna mwaka mwamba huyu alitoa album 12 karibu kila mwezi alikuwa anatoa album moja.

Franco alifariki mwaka 1989, alikuwa na umri wa miaka 51, vyanzo vingi vinasema Franco alifariki kutokana na ugonjwa wa UKIMWI. Katika uhai wake Franco alibahatika kupata watoto 18, Watoto wakike walikuwa 17 na mmoja wakiume.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live