Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dimpoz: Niliamini naweza kusimama bila Diamond

Mondi Dimpoz (1).jpeg Dimpoz: Niliamini nitasimama bila Diamond

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Supastaa wa Bongo Fleva, Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz amesema kuwa aliamini anaweza kusimama na kuwa staa bila ya kushikwa mkono na Diamond Platnumz.

Itakumbukzwa kuwa, Dimpoz na Diamond walikuwa marafiki tangu wakiwa hawajawa mastaa wakubwa lakini baadae walitofautiana kabla ya kupata tena mwaka jana.

"Mimi na yeye hatuna kolabo lakini tulikutana kwenye nyimbo ya mtu mfano ya Dully utamu, na ya Victoria kimani na tukakutana tena kwenye project ya kigoma lakini hatuna kwamba hii ni mimi yangu na yeye kwa sababu nilikuwa naamini naweza kusimama mwenyewe," amesema Dimpoz.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live