Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Babu Tale: Wafanyakazi wa Basata wana roho mbaya

BABU TALE 1024x661.jpeg Mbunge wa Morogoro Kusini, Hamis Taletale 'Babu Tale'

Mon, 6 Jun 2022 Chanzo: Tanzania

Mbunge wa Morogoro Kusini, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ amewachana baadhi ya wafanyakazi wa Baraza la Sanaa la taifa kwa kitendo cha kufungia nyimbo za wasanii badala ya kuwapa elimu ya kisheria.

Babu Tale ameyasema hayo leo Juni 6, 2022 alipokuwa akichangia hoja Bungeni ambapo alianza kwa kushusha dua kabla ya kufikisha ujumbe huo alioukusudia.

“Kwanza nimpongeze Rais, nimpongeze Waziri Mchengerwa kwa kazi nzuri anayoifanya lakini baadhi ya watumishi wake wana roho mbaya. Wao wanachojua ni kuwafungia tu wasanii badala ya kuwapa elimu.

“Hawajui msanii anatumia muda kutunga kitu wakiona msanii fulani hana maslahi naye wanamwacha lakini yule ambaye wana maslahi naye wanamfungia,”alisema Babu Tale.

Chanzo: Tanzania
Related Articles: