Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba Levo: Alikiba aache umwinyi

Alikiba Diamond .jpeg Baba Levo: Alikiba aache umwinyi

Mon, 17 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msani wa Bongo Fleva na chawa maarufu, Baba Leo ameonyesha kufurahishwa na kile kinachoendelea baina ya manguli wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba na hasimu wake Diamond Platnumz.

Akiwa kwenye mahojiano na waandishi wa habari, Baba Levo ambaye pia ni mtangazaji wa Wasafi FM amesema amefurahishwa na kitendo cha Kiba kuanza kutangaza kazi zake baada ya kuona promo zimekuwa zikiwasaidia wasanii ku-push kazi zao na kuwafikia mashabiki zao.

"Alikiba anapromote nyimbo sababu amegundua Umwinyi unampoteza kimuziki, zamani alikuwa akitoa nyimbo analala anasubiri mashabiki wampiganie lakini sasa hivi unaona anazunguuka kwenye maredio na maklabu kutangaza nyimbo.

"Kiba alikuwa hataki machawa sasa hivi kamganda Mwijaku kila anapoenda yote ni kupambana kutangaza nyimbo na ndivyo muziki unataka," amesema Baba Levo.

Ikumbukwe kuwa Diamond ametangaza kuachia ngoma baada ya ngoma huku kiba naye akitangaza kuachia mawe mfululizo kila baada ya siku kadhaa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: