Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amkeni ya Nay wa Mitego yafungiwa

Nay 9 WA0007 Amkeni ya Nay wa Mitego yafungiwa

Sat, 29 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa inayosambaa hii leo Julai 29, 2023 kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) inaeleza kufungiwa kwa wimbo wa Amkeni wa Nay wa Mitego kwa kile kinachoelezwa kwamba unachonganisha wananchi na Serikali yao.

Barua hiyo ya TCRA inazuia wimbo huo kupigwa kwenye mitandaoni ya kijamii na vyombo vya Habari.

Nay wa Mitego ameposti barua hiyo kwenye ukurasa wake wa Twitter au X ikionesha imesainiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), John Daffa.

Baada ya kutoka kwa wimbo huo, hivi karibuni Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lilieleza kuwa maudhui ya wimbo huo yana mwelekeo wa kutaka wananchi wasiwe na imani na Serikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live